TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA KUJITOLEA BAKWATA MKOA WA MWANZA

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mwanza linatangaza nafasi za kujitolea kwa vijana kupitia Jumuiya yake ya vijana inayojulikana kama JUVIKIBA (Jumuiya ya Vijana wa Kiislamu wa BAKWATA).

Nafasi zinazotangazwa ni:

1. Mwenyekiti wa JUVIKIBA – Mkoa

Majukumu:

  1. Kuongoza na kusimamia vikao vya JUVIKIBA ngazi ya mkoa.
  2. Kutoa mwelekeo na dira ya jumuiya ya vijana ndani ya BAKWATA.
  3. Kusimamia utekelezaji wa mipango, mikakati na shughuli za jumuiya.
  4. Kuwakilisha JUVIKIBA katika mikutano, warsha, semina na matukio mbalimbali.
  5. Kuhamasisha na kushirikisha vijana katika shughuli za kijamii, kiuchumi na kiimani.
  6. Kubuni na kusimamia miradi ya maendeleo ya vijana katika nyanja za kijamii na kiuchumi.
  7. Kushauriana na viongozi wa BAKWATA mkoa kuhusu maendeleo ya jumuiya ya vijana.

Sifa za Muombaji:

  1. Awe Muislamu mwenye maadili mema, uadilifu na hofu ya Mungu.
  2. Awe na umri kati ya miaka 20 hadi 40.
  3. Awe na uzoefu wa uongozi au ushiriki wa kazi katika jumuiya/taasisi za vijana.
  4. Awe na uwezo wa kuhamasisha na kuongoza vijana kwa njia chanya.
  5. Awe na elimu ya dini ya Kiislamu na elimu ya sekondari kuanzia kidato cha 4 na kuendelea.
  6. Elimu ya dini ya Kiislamu itapewa kipaumbele.
  7. Awe na uwezo wa kubuni na kusimamia miradi ya kijamii, kidini  na kiuchumi.

2. Katibu wa JUVIKIBA – Mkoa

Majukumu:

  • Kuandaa ajenda na kumbu kumbu za vikao vya jumuiya.
  • Kuhifadhi na kusimamia nyaraka zote muhimu za JUVIKIBA.
  • Kuratibu shughuli zote za kila siku za jumuiya kwa ufanisi.
  • Kuandaa na kuwasilisha ripoti mbalimbali za utendaji kwa uongozi wa mkoa.
  • Kufuatilia utekelezaji wa maazimio ya vikao na miradi ya JUVIKIBA.
  • Kushirikiana kwa karibu na Mwenyekiti kuhakikisha jumuiya inatekeleza majukumu yake kwa mafanikio.
  • Kuwasiliana na wadau mbalimbali kwa niaba ya jumuiya.
  • Kubuni na kusimamia miradi ya kijamii na kiuchumi kwa ajili ya maendeleo ya vijana.
  • Kuandaa maandiko ya miradi, barua rasmi, taarifa na ripoti.

Sifa za Muombaji:

  • Awe Muislamu mwenye nidhamu, maadili na moyo wa kujitolea.
  • Awe na umri kati ya miaka 20 hadi 40.
  • Awe na elimu ya dini ya Kiislamu na elimu ya sekyula (kidato cha nne na kuendelea).
  • Elimu ya Astashahada (Certificate) na kuendelea ya fani yoyote itapewa kipaumbele..
  • Awe na ujuzi mzuri wa kutumia kompyuta (MS Word, Excel, Power Point, Publisher, Email n.k).
  • Awe na uzoefu wa uongozi au kazi za jumuiya ni faida ya ziada.
  • Awe na uwezo wa kubuni na kusimamia miradi ya kijamii, kidini na kiuchumi.

3. Mweka Hazina wa JUVIKIBA – Mkoa

Majukumu:

  • Kusimamia mapato na matumizi yote ya fedha za jumuiya kwa uadilifu na uwazi.
  • Kutunza kumbukumbu za fedha na vielelezo vyote vya matumizi.
  • Kuandaa taarifa za fedha na kuziwasilisha kwenye vikao vya jumuiya.
  • Kushirikiana na viongozi wa jumuiya kupanga na kusimamia bajeti ya kila mwaka ya Jumuiya.
  • Kusimamia vyanzo vya mapato vya jumuiya.
  • Kuhakikisha fedha zote zinatumika kwa kufuata taratibu zilizowekwa.
  • Kushiriki katika kubuni na kutekeleza miradi ya kiuchumi ya vijana.

Sifa za Muombaji:

  • Awe Muislamu mwaminifu, mwenye hofu ya Mungu na uadilifu wa hali ya juu.
  • Awe na umri kati ya miaka 20 hadi 40.
  • Awe na elimu ya dini na elimu ya sekyula (Kidato cha 4 na kuendelea)
  • Elimu ya fedha, uhasibu au uendeshaji wa miradi ni faida ya ziada.
  • Awe na uwezo wa kutumia kompyuta, hususan programu za kutunza taarifa za fedha (mf. Excel).
  • Awe na uzoefu katika shughuli za fedha au kazi za kijumuiya.
  • Awe na uwezo wa kushiriki katika kubuni na kusimamia miradi ya kijamii na kiuchumi.

4. Mwenyekiti wa Idara ya Wanawake – JUVIKIBA Mkoa

Majukumu:

  • Kuongoza Idara ya Wanawake ndani ya JUVIKIBA Mkoa.
  • Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa shughuli zote zinazohusu wanawake ndani ya jumuiya.
  • Kuwakilisha wanawake wa JUVIKIBA kwenye mikutano na vikao vya jumuiya.
  • Kuhamasisha wanawake kushiriki katika shughuli za kijamii, kiuchumi na kiimani.
  • Kubuni na kusimamia miradi ya maendeleo ya wanawake.
  • Kushauriana na uongozi wa JUVIKIBA kuhusu mahitaji na masuala ya wanawake vijana.

Sifa za Muombaji:

  • Awe mwanamke Muislamu mwenye maadili mema, heshima na uadilifu.
  • Awe na umri kati ya miaka 20 hadi 40.
  • Awe na elimu ya dini na elimu ya sekyula kaunzia kidato cha 4 na kuendelea; elimu ya dini ya Kiislamu ni kipaumbele.
  • Awe na uzoefu wa uongozi au ushiriki wa kazi katika jumuiya au taasisi za wanawake.
  • Awe na uwezo wa kubuni na kusimamia miradi ya wanawake ya kijamii na kiuchumi.

5. Katibu wa Idara ya Wanawake – JUVIKIBA Mkoa

Majukumu:

  • Kuandaa ajenda na kumbu kumbu za vikao vya Idara ya Wanawake.
  • Kuhifadhi na kusimamia nyaraka zote za idara.
  • Kuratibu shughuli za kila siku za idara ya wanawake.
  • Kuandaa ripoti na taarifa za utendaji na kuziwasilisha kwa viongozi wa JUVIKIBA.
  • Kusaidia katika maandalizi na uendeshaji wa miradi na shughuli za wanawake.
  • Kubuni na kusimamia miradi ya wanawake yenye tija kwa jamii na kiuchumi.

Sifa za Muombaji:

  • Awe Mwananmke Muislamu mwenye nidhamu, maadili na moyo wa kujitolea.
  • Awe na umri kati ya miaka 20 hadi 40.
  • Awe na elimu ya dini ya Kiislamu na elimu ya sekyula (kidato cha nne na kuendelea).
  • Elimu ya Astashahada (Certificate) na kuendelea ya fani yoyote itapewa kipaumbele..
  • Awe na ujuzi mzuri wa kutumia kompyuta (MS Word, Excel, Power Point, Publisher, Email n.k).
  • Awe na uzoefu wa uongozi au kazi za jumuiya ni faida ya ziada.
  • Awe na uwezo wa kubuni na kusimamia miradi ya kijamii, kidini na kiuchumi

6. Mweka Hazina wa Idara ya Wanawake – JUVIKIBA Mkoa

Majukumu:

  • Kusimamia mapato na matumizi ya fedha za Idara ya Wanawake kwa uadilifu.
  • Kutunza kumbukumbu zote za fedha na vielelezo vinavyohusiana.
  • Kuandaa taarifa za kifedha na kuziwasilisha kwenye vikao vya idara.
  • Kusimamia vyanzo vya mapato, na bajeti za miradi ya wanawake.
  • Kushiriki katika kubuni na kutekeleza miradi ya kiuchumi kwa wanawake vijana.

Sifa za Muombaji:

  • Awe Wamanmke Muislamu mwaminifu, mwenye hofu ya Mungu na uadilifu wa hali ya juu.
  • Awe na umri kati ya miaka 20 hadi 40.
  • Awe na elimu ya dini na elimu ya sekyula (Kidato cha 4 na kuendelea)
  • Elimu ya fedha, uhasibu au uendeshaji wa miradi ni faida ya ziada.
  • Awe na uwezo wa kutumia kompyuta, hususan programu za kutunza taarifa za fedha (mf. Excel).
  • Awe na uzoefu katika shughuli za fedha au kazi za kijumuiya.
  • Awe na uwezo wa kushiriki katika kubuni na kusimamia miradi ya kijamii na kiuchumi

Namna ya Kutuma Maombi:
Waombaji wanatakiwa kuwasilisha:

  • Barua ya maombi ikieleza nafasi anayoiomba na sababu za kuomba.
  • Nakala ya CV (Wasifu binafsi) yenye maelezo ya elimu, uzoefu, na mawasiliano.
  • Ambatanisha Picha yako ya Passport Size kwenye barua ya maombi.

Maombi yatumwe kupitia barua pepe:
📧 info@bakwatamwanza.or.tz  / b2jhms@gmail.com
AU
Yaletwe moja kwa moja katika:
Ofisi za BAKWATA Mkoa wa Mwanza

S.L.P 1679

Mtaa wa Unguja, Mwanza Tanzania

Mwisho wa kutuma maombi: 20 Aprili 2025

Kwa maelezo zaidi, wasiliana na:
+255 748 089 348

ZINGATIA: Nafasi hizi ni za kujitolea, utapaswa kufanya kazi kwa moyo wa uzalendo, imani na hamasa ya kuleta maendeleo kwa vijana wa Kiislamu mkoani Mwanza.

TANGAZO HILI LIMETOLEA NA OFISI YA SHEIKH WA MKOA WA MWANZAApril 13, 2025

About the Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like these

X